Mikoa ya Kodivaa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mikoa ya Kodivaa (Kifaransa: Régions de Côte d’Ivoire) ni ngazi ya pili ya ugatuzi nchini Kodivaa. Nchi imegawanywa katika wilaya 14 ambazo ni ngazi ya kwanza ya ugatuzi. Wilaya mbili ni miji iliyoandaliwa kama wilaya huru na wilaya 12 za kawaida zinagawanyika katika mikoa 31.
Mikoa na wilaya zisizo huru, imegawanywa katika tarafa 108 ambazo ni ngazi ya tatu ya ugatuzi.