Mhusika (kwa Kiing. character) katika fasihi simulizi ni kiumbehai au kisichokuwa na uhai, anayechorwa na msanii wa kazi ya fasihi kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa hadhira.[1]

Mfano wa wahusika hao ni binadamu, wanyama, miti, mawe, mapango n.k.

Aghalabu wahusika wa fasihi simulizi ni wengi kwani wanahusisha viumbe wote, wenye uhai na wasiokuwa na uhai.

Kuna namna mbalimbali za kuainisha wahusika[2]

1. Wahusika wakuu. Hawa hutawala visa katika kazi za kifasihi maana hadithi huwahusu wao na athari yao ni kubwa hivi kwamba kama hawangekuwa, basi nayo hadithi haingekuwa. Wakitenda mema, huitwa "nguli" ilhali wa maovu huitwa "hasidi".

2. Wahusika wadogo/wasaidizi ambao huwa karibu na wakuu ili kusaidia kuwaelewa vyema. Hukuza msuko/ploti na maudhui.

3. Wahusika wajenzi. Hawa huwa karibu na wahusika wakuu na wadogo kwani husaidia kuzijenga sifa na umuhimu wa wahusika wakuu na wadogo.

4. Wahusika bapa hushikilia misimamo yao katika kazi husika. Hawabadiliki. Wakiwa hasidi hubaki hivyo hadi mwisho na wakiwa nguli vivyo hivyo.

5. Wahusika duara huakisi tabia zote za kibinadamu, njema na mbaya.

Ni vyema kufahamu kuwa mhusika mmoja anaweza kuingia katika makundi tofautitofauti ya uhusika.

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.