Mgongo kati wa Bahari Hindi
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mgongo kati wa Bahari Hindi (kwa Kiingereza: Central Indian Ridge) ni safu ya milima chini ya maji ya Bahari Hindi yenye mwelekeo kutoka kusini hadi kaskazini.
Sawa na migongo mingine kati ya bahari huo umetokea pale ambako mabamba ya gandunia yaani mapande ya ganda la Dunia hukutana chini ya bahari. Kwenye mstari ambako mabamba hayo yanakutana kuna ufa unaoruhusu kupanda juu kwa magma na lava kutoka koti ya Dunia kama mstari wa volkeno chini ya maji. Miamba hiyo kwenye hali ya kiowevu inaganda inapotoka nje na kuingia katika maji ya bahari, hivyo kujenga safu ndefu ya milima.
Mgongo kati ya Bahari Hindi unatenganisha Bamba la Afrika na mabamba ya Uhindi na Australia.
Mabamba hayo yanatawanya kwenye mgongo kati wa Bahari Hindi yakiachana kila mwaka mnamo milimita 30-50.[1]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.