![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/e/e0/%2522Seawise_Giant%2522_-_Singapore%252C_1990.jpg/640px-%2522Seawise_Giant%2522_-_Singapore%252C_1990.jpg&w=640&q=50)
Meli kubwa duniani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Meli kubwa duniani siku hizi ni meli za mizigo hasa zinazobeba mafuta ya petroli au kontena, lakini pia meli za abiria zinazobeba watalii kwa burudani. Kuna pia meli chache zenye kusudi maalumu kama MS Pioneering Spirit ambayo ni meli kubwa ya winchi kwa ujenzi baharini.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/e/e0/%22Seawise_Giant%22_-_Singapore%2C_1990.jpg/640px-%22Seawise_Giant%22_-_Singapore%2C_1990.jpg)
Meli kubwa kabisa iliyojengwa hadi sasa ilikuwa Seawise Giant yenye tani GT 564,763 na urefu wa mita 458. Ilitengenezwa mwaka 1974-1979 nchini Japani kwa kampuni ya Kigiriki na kurefushwa baadaye hadi kufikia mita 458. Kutokana na ukubwa wake haukuweza kupita wala katika Mfereji wa Suez wala katika Mfereji wa Kiingereza. Miaka yake ya mwisho ilitumiwa kama tangi ya mafuta tu bila kusafiri tena. Mwaka 2009 ilivunjika.