From Wikipedia, the free encyclopedia
Midumu-mwitu ni mimea inayokula wadudu kwa kutumia mtego kwa umbo wa kikombe kirefu au mdumu wenye maji ndani. Mimea hii ni wana wa familia mbili: Nepenthaceae au midumu-mwitu ya Dunia ya Kale na Sarraceniaceae au midumu-mwitu ya Dunia Mpya (familia Cephalotaceae ina spishi moja tu). Imedhaniwa kuwa mitego ya midumu-mwitu yenye maji ndani iliibuka kutoka matawi yaliyojikunja, huku mabadiliko ya viumbe yakipendelea matawi yenye michimbuko mikubwa zaidi katika kipindi cha miaka mingi.
Mdumu-mwitu | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mdumu-mwitu (Sarracenia flava) | ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Jenasi 5:
|
Hata hivyo, baadhi ya midumu-mwitu wa jenasi kama ile ya Nepenthes wanajumuishwa katika kikundi tofauti cha mimea wenye matawi kama karatasi yenye gundi. Hili linaonyesha kuwa mtazamo kuwa midumu mwitu iliibuka kutoka matawi yaliyojikunja huenda hukawa si wa kweli.
Bila kujali jinsi mmea huu ulivyobadilika, wadudu wanaotambaa na wanaoruka ikiwemo nzi huvutiwa kwa mchimbuko huo ulioundwa na tawi, mara nyingi kwa rangi na maji yenye sukari. Pande za tawi huenda zikawa zinateleza na zimeumbwa kwa njia inayowafanya wadudu washindwe kutoka pindi wanapoingia ndani.
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mdumu mwitu kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.