From Wikipedia, the free encyclopedia
Wadudu mikia-mitatu ni arithropodi wadogo wa oda Thysanura (thysanos = nyoya yabisi, ura = mkia) katika nusungeli Apterygota (maana: bila mabawa) ya ngeli Insecta (wadudu wa kweli). Mikia mitatu ya wadudu hawa ni kwa kweli serki ndefu mbili na epiprokti iliyorefuka (“pingili” ya 11 ya fumbatio). Kiwiliwili chao ni bapa chenye umbo la yai au kimerefuka. Vipapasio ni kinamo na vipande vya mdomo ni vifupi na havikubobea. Hawana macho au macho ni madogo tu. Kiunzi-nje cha wadudu hawa si ngumu na kimefunikika kwa vigamba ambavyo vina rangi ya fedha mara nyingi. Kwa sababu ya hiyo na mwendo wao unaofanana na kuogelea, spishi kadhaa huitwa kisamaki-fedha. Kwa kawaida huonekana katika mazingira manyevu, pengine katika mazingira makavu. Visamaki-fedha huishi mara nyingi katika nyumba ambapo hula nafaka, lahamu, karatasi, wanga katika nguo, vitambaa vya rayoni na nyama iliyokauka. Spishi nyingine huishi katika mapango au katika vichuguu.
Mdudu mikia-mitatu | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
“Kisamaki-fedha” (Lepisma saccharina) | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Familia 5:
| ||||||||||||||
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mdudu Mikia-mitatu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.