Mbwa ni wanyama mbuai wa familia Canidae, lakini takriban spishi zote za Afrika zinaitwa bweha au mbweha.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Mbwa |
Mbwa-mwitu wa Ulaya |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Nusufaila: |
Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
|
Ngeli: |
Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
|
Oda: |
Carnivora (Wanyama mbua)
|
Nusuoda: |
Caniformia (Wanyama kama mbwa)
|
Familia: |
Canidae Fischer, 1817 |
|
Ngazi za chini |
Jenasi 12:
- Atelocynus Cabrera, 1940
- Canis Linnaeus, 1758
- Cerdocyon C.E.H. Smith, 1839
- Chrysocyon C.E.H. Smith, 1839
- Cuon Hodgson, 1838
- Lupulella Hilzheimer, 1906
- Lycalopex Burmeister, 1854
- Lycaon Brookes, 1827
- Nyctereutes Temminck, 1839
- Otocyon Müller, 1836
- Speothos Lund, 1839
- Urocyon Baird, 1857
- Vulpes Frisch, 1775
|
Funga
Ukubwa wa spishi za mwitu unatofautiana kutoka 24 sm (fenek) mpaka 2 m ( mbwa mwitu wa Ulaya (kadiri ya vipimo kwa mbwa-kaya ni 9.5-250 sm).
Mbwa wa familia Canidae hupatikana mabara yote isipokuwa Antaktika.
Wanyama hawa wana pua ndefu na miguu mirefu na mkia wa manyoya. Rangi yao ni kijivu, kahawia au hudhurungi; kwa kawaida tumbo ni jeupe.
Spishi nyingine zinatokea misituni na nyingine zinatokea maeneo wazi. Mbwa hukamata mawindo aina yoyote lakini ukubwa wa mawindo unafuatana na ukubwa wa spishi ya mbwa. Hata hivyo, spishi zinazoishi kwa makundi, kama mbwa-mwitu wa Afrika, zinaweza kukamata windo kubwa sana kuliko wao wenyewe. Spishi kadhaa hufugwa na binadamu, hususan mbwa-kaya.
- Canis anthus, Mbwa-mwitu Dhahabu au Bweha wa Mbuga (Common or African Golden Wolf)
- Canis lupus, Mbwa-mwitu wa Ulaya (Grey Wolf)
- Canis l. familiaris, Mbwa-kaya (Domestic Dog)
- Canis simensis, Mbwa-mwitu Habeshi (Ethiopian Wolf, Abyssinian Wolf, Simien Fox au Simien Jackal)
- Lupulella adusta, Bweha Miraba (Side-striped jackal)
- Lupulella mesomelas, Bweha Mgongo-mweusi au Bweha Shaba (Black-backed Jackal)
- Lycaon pictus, Mbwa-mwitu wa Afrika (African Wild Dog, African Sun Wolf au African Hunting Dog)
- Otocyon megalotis, Bweha Masikio (Bat-eared Fox)
- Otocyon m. megalotis, Bweha Masikio Kusi
- Otocyon m. virgatus, Bweha Masikio Mashariki
- Vulpes cana, Bweha wa Blanford (Blanford's Fox)
- Vulpes chama, Bweha Kusi (Cape Fox)
- Vulpes pallida, Bweha wa Saheli (Pale Fox)
- Vulpes rueppelli, Bweha wa Rüppell (Rüppell's Fox)
- Vulpes vulpes, Bweha Mwekundu
- Vulpes v. barbara, Bweha Mwekundu wa Barbari (Barbary fox)
- Vulpes v. niloticus, Bweha Mwekundu wa Misri (Nile fox)
- Vulpes zerda, Feneki au Bweha-jangwa (Fennec Fox)
Bweha miraba
Mbwa-mwitu wa Senegali
Mbwa-mwitu mashariki
Mbwa-kaya
Mbwa-mwitu wa Misri
Bweha mgongo-mweusi
Mbwa-mwitu Habeshi
Mbwa-mwitu wa Afrika
Bweha masikio
Bweha wa Blanford
Feneki
Short-eared dog (Mbwa masikio-mafupi)
Coyote (Mbwa-nyika)
Dingo
Dingo wa Nyugini
Crab-eating dog (Bweha mla-kaa)
Maned worlf (Mbwa manyonya-marefu)
Dhole
Culpeo
Raccoon dog (Mbwa-rakuni)
Bush dog
Grey fox (Bweha kijivu)
Arctic fox (Bweha-akitiki)
Red fox (Bweha mwekundu)