From Wikipedia, the free encyclopedia
Mbuni wa Kawaida ni ndege wakubwa wasioruka wa familia Struthionidae wenye asili ya bara la Afrika.
Mbuni wa kawaida | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mbuni Masai | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Nususpishi 4:
| ||||||||||||||
Msambazo wa mbuni katika Afrika | ||||||||||||||
Mbuni wa kawaida wako katika ngeli ndogo ya Palaeognathae pamoja na ndege wengine kama Kiwi na Emu. Ndege hawa wenye shingo na miguu mirefu huweza kukimbia karibu maili 43 kwa saa. Ndege hawa ni wakubwa kuliko aina zote za ndege na hutaga mayai makubwa kuliko ndege wa aina yoyote duniani.
Chakula chao kikuu ni aina mbalimbali za mimea. Kawaida huishi katika makundi ya ndege 5 hadi 50. Wakiwa hatarini, ndege hwa hujificha kwa kulala sambamba ardhini au kukimbia. Wakati mwingine hujilinda kwa kushambulia kwa teke la miguu yake yenye nguvu.
Mbuni wa kawaida hufugwa duniani kote, hasa kwa manyoya yake, ambayo yanapendeza sana kwa rangi zake. Ngozi yake hutumiwa kutengeneza bidhaa za ngozi na nyama yake huuzwa kwa walaji nyama.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mbuni wa Kawaida kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.