Shemasi (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kigiriki: διάκονος, diákonos[1] maana yake "mtumishi", "msaidizi", "mhudumu", au "mjumbe".[2]) ni kiongozi wa Kanisa anayeunganisha wenye daraja za juu na walei.

Thumb
Shemasi wa Kanisa Katoliki huko Polandi akiimba mbiu Exsultet usiku wa Pasaka.
Thumb
Shemasi wa Kiorthodoksi katika mavazi yake rasmi.

Hii ni kwa sababu ushemasi ni daraja ya tatu na ya mwisho katika Kanisa Katoliki na madhehebu mengine kadhaa ya Ukristo. Unatolewa na Askofu kwa kumwekea muumini mikono na kumuombea ili atoe vizuri huduma ya Neno la Mungu, ya liturujia na ya matendo ya upendo. Unaweza kutolewa kwa namna ya kudumu au kama hatua ya kuelekea daraja ya upadri.

Katika Kanisa la Moravian ushemasi ni ngazi ya kwanza ya uchungaji.

Katika historia ya Kanisa mashemasi waliotoa mchango mkubwa, mara nyingi kwa kukamilisha ushuhuda wao kwa kumfia Yesu.

Kati yao maarufu zaidi ni Laurenti Mfiadini, Efrem wa Syria, na Fransisko wa Asizi.

Katika Biblia

Imezoeleka kusema ushemasi ulianzishwa na Mitume walipoweka viongozi saba wenye kusema Kigiriki kuwasaidia katika kuongoza Kanisa la Yerusalemu[3][4]. Wa kwanza wao alikuwa Stefano [5]. Hata hivyo wataalamu wengine wanasema hao saba hawakuwa mashemasi tu.

Kwa vyovyote cheo cha ushemasi kinazungumziwa na Agano Jipya, hasa katika Nyaraka za Kichungaji, Mtume Paulo anapotaja sifa za shemasi (1Tim 3:1-13).

Tanbihi

Viungo vya nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.