![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/0/08/Landscape_marble_skyline.jpg/640px-Landscape_marble_skyline.jpg&w=640&q=50)
Marumaru
From Wikipedia, the free encyclopedia
Marumaru (pia: marmar - kutoka Kiarabu مرمر; kwa Kiingereza: marble) ni mwamba wa gange uliobadilika kutokana na joto na shindikizo ndani ya ganda la dunia katika kipindi cha miaka milioni kadhaa. Kikemia ni hasa CaCO3.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/0/08/Landscape_marble_skyline.jpg/640px-Landscape_marble_skyline.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/de/Venus_de_Milo_Louvre_Ma399-02b.jpg/120px-Venus_de_Milo_Louvre_Ma399-02b.jpg)
Ni jiwe gumu sana linalopatikana katika rangi mbalimbali.
Hupendwa sana kama jiwe la ujenzi, hasa kama ni nyeupe. Kama ni haba katika eneo fulani hutumiwa kama mapambo tu, kama vile kwa kufunika kuta.
Jiwe lenye rangi mbalimbali hutumiwa kwa sakafu katika majengo muhimu au kama mapambo ya kuta za ndani.
Tangu kale marumaru ilitumiwa pia kwa kuchonga sanamu.