Luxemburg (mji)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Luxemburg (Kiluxemburg: Lëtzebuerg, Kifaransa:Luxembourg; Kijerumani: Luxemburg) ni mji mkuu wa Utemi wa Luxemburg katika Ulaya ya Kati.
Ukweli wa haraka Nchi, Wilaya ...
Luxemburg | |
Nchi | Luxemburg |
---|---|
Wilaya | Luxembourg |
Canton | Luxembourg |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 76 688 |
Funga
Mji ulikuwa na wakazi 76,420 mnamo mwaka 2005. Uko kusini mwa nchi ambako mito ya Alzette na Pétrusse inaungana.
Mji wa Luxemburg ni kati ya miji tajiri za Ulaya. Uchumi umekua sana upande wa benki na biashara. Luxemburg ni pia moja kati ya miji mikuu ya Umoja wa Ulaya pamoja na Brussels na Strasbourg. Mahakama Kuu ya Ulaya ina makao makuu hapa pia Mamlaka Kuu ya Ukaguzi wa Ulaya na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya.
Mji wa Kale ya Luxemburg uliingizwa na UNESCO katika orodha ya urithi wa dunia.