Lemuri-sufu (kutoka Kiingereza: woolly lemur) ni spishi za lemuri wa jenasi Avahi katika familia Indriidae. Kama lemuri wote wanatokea Madagaska tu. Manyoya yao ni laini na ya kusokotwa kama sufu. Wana rangi ya kahawiakijivu hadi kahawianyekundu na mkia una rangi ya kahawiamachungwa. Iko rangi ya nyeupe nyuma ya mapaja. Mwili wa wanyama hawa una urefu wa sm 30-50 na uzito wao ni g 60-1200, kwa hivyo wao ni spishi ndogo kuliko nyingine za familia hii. Hula majani hasa na pengine matumba na maua.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Lemuri-sufu |
Lemuri-sufu mashariki |
Uainishaji wa kisayansi |
Domeni: |
Eukaryota (Viumbe walio na seli zenye kiini)
|
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Ngeli: |
Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
|
Oda: |
Primates (Wanyama wanaofanana kiasi na binadamu)
|
Nusuoda: |
Strepsirrhini (Wanyama wanaofanana zaidi na lemuri)
|
Oda ya chini: |
Lemuriformes (Wanyama kama kima)
|
Familia ya juu: |
Lemuroidea (Lemuri)
|
Familia: |
Indriidae (Lemuri walio na mnasaba na indri)
|
Jenasi: |
Avahi Jourdan, 1834 |
|
Ngazi za chini |
Spishi 9
- A. betsileo Andriantompohavana et al., 2007
- A. cleesei Thalmann & Geissmann, 2005
- A. laniger (Gmelin, 1788)
- A. meridionalis Zaramody et al., 2006
- A. mooreorum Lei, 2008
- A. occidentalis Lorenz von Liburnau, 1898
- A. peyrierasi Zaramody et al., 2006
- A. ramanantsoavanai Zaramody et al., 2006
- A. unicolor Thalmann & Geissmann, 2005
|
Funga