![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/1d/Leeds_Rathaus.jpg/640px-Leeds_Rathaus.jpg&w=640&q=50)
Leeds
From Wikipedia, the free encyclopedia
Leeds ni mji katika kaskazini ya Uingereza na mji mkubwa wa tatu nchini mwenye wakazi 458,000 mjini penyewe ambao pamoja na rundiko la "Metropolitan Borough City of Leeds" wanafikia 700,000.
Ukweli wa haraka Nchi, Mkoa ...
Jiji la Leeds | |
Mahali pa mji wa Leeds katika Uingereza |
|
Majiranukta: 53°47′59″N 1°32′57″W | |
Nchi | Uingereza |
---|---|
Mkoa | Yorkshire na Humber |
Wilaya | West Yorkshire |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 761,100 |
Tovuti: www.leeds.gov.uk |
Funga
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/1d/Leeds_Rathaus.jpg/640px-Leeds_Rathaus.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/8/85/Briggate%2C_Leeds.jpg/640px-Briggate%2C_Leeds.jpg)
Leeds ilikua kuwa mji mkubwa wakati wa mapinduzi ya viwandani kama kitovu cha viwanda vya vitambaa na nguo. Siku hizi biashara kama benki na huduma za kila aina zimechukua nafasi ya kwanza.
Leeds imejulikana pia kutokana na Chuo Kikuu chake kilichoundwa mwaka 1904. Wanafunzi wengi kutoka Afrika walichukua masomo ya juu hapa wanaojulikana zaidi ni waandishi Wole Soyinka kutoka Nigeria na Ngũgĩ wa Thiong'o wa Kenya.
Timu ya soka ya Leeds United imekuwa kati ya klabu muhimu za uingereza kwa miaka mingi.