From Wikipedia, the free encyclopedia
Lecrae Moore (amezaliwa 9 Oktoba, 1979) ni msanii wa Kikristo[1] mwenye mkataba na Reach Records.[2]
Lecrae | |
---|---|
Lecrae na Akon, mnamo 2013 | |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Lecrae Moore |
Aina ya muziki | Kikristo, Nyimbo za Kikristo |
Kazi yake | Mwanamuziki |
Studio | Reach Records |
Tovuti | http://www.reachrecords.com/ |
Lecrae anaishi mjini Atlanta, Georgia akiandaa matukio mbalimbali ya muziki, akijitolea kufanya kazi katika jela ya vijana, kujishirikisha katika shirika la Kids Across America Kamps huko Branson, Missouri na akijishughulisha na Reachlife Ministries.[3] Pia, yeye ni mwanachama wa 116 Clique, Lecrae anahubiri Injili katika vyuo vikuu mbalimbali na kumbi mbalimbali za jamii.
Lecrae amepokea uchaguzi wa kuwa mshindani kwa tuzo mbili katika tuzo za kila mwaka za GMA Dove. Alipata uchaguzi kwa wimbo wake Jesus Muzik,aliomshirikisha Trip Lee na kwa albamu yake After the Music Stops[4]. Yeye ,hivi majuzi,alikuwa amechaguliwa kama mshindani kwa tuzo ya Albamu ya Sanaa ya Rap ya Mwaka katika tuzo za arubaini za GMA Dove. Magazeti mbalimbali,likiwemo Rapzilla[5] yameaona na kusifu mtindo wake tofauti na albamu yake ya pili After the Music Stops iliitwa "mojwapo ya albamu bora sana ya 2006[6]". Nyimbo zake zinaonyesha werevu wake lakini zinahakikisha ujumbe umewasilishwa.
Katika muziki wake, Lecrae anatumia neno "Crunk" kwa kumaanisha hisia nzuri anayohisi Mkristo.[7] 8 Oktoba 2008, albamu ya tatu ya Lecrae, Rebel, iliingia chati ya Billboard ikwa # 60,huku ikiwa imenunuliwa na watu 9,800. Rebel ikawa # 3 katika iTunes na kushikilia nafasi ya kwanza katika chati ya Kikristo ya Billboard kwa wiki mbili,albamu ya rap ya kwanza kufanya hivyo. Lecrae ana video nne vya nyimbo zake:Jesus Muzik, Praying For You, Don't Waste Your Life, ambayo ilishinda Video ya Mwaka katika tuzo za GMC na hapo Oktoba 2009 alitoa video ya wimbo wake Go Hard.
Alizaliwa Houston, Texas na akalelewa na mama pekee bila baba, alikuwa Mkristo akiwa na umri wa miaka 19. Lecrae alianza kuimba juu ya imani yake na kuwa mwanzilishi wa Reach Records akiwa na umri wa miaka 25. Mwaka 2005, alitoa albamu yake ya Real Talk[8] The album gained critical acclaim and charted at #29 on the Billboard Gospel albums chart.[9] kwa kurekodia huko Reach Records.[10] Albamu hiyo ilipata sifa ikawa #29 kwenye chati ya Billboard ya albamu za Kikristo.[11]
Baada ya ufanisi wa Real Talk,Lecrae alitoa albamu yake ya pili ya studio mnamo 15 Agosti ,2006,albamu hiyo ilikuwa #5 katika chati ya Billboard ya albamu za Kikristo na #16 katika chati ya Billboard Heatseeker.[12] Albamu hii ilichaguliwa kuwa mshindani katika tuzo ya Dove na vilevile wimbo wake Jesus Musik ulichaguliwa.
Tarehe 8 Oktoba 2008, albamu ya tatu,Rebel, iliingia chati ya Billboard katika nafsi ya 60 ikiwa imenunuliwa na watu 9,800.Albamu hiyo ilipata sifa nyingi kabisa kwa muziki ya aina hiyo.Jesusfreakhideout ilisema,"Katika ulimwengu wa muziki,albamu hii ni nzuri sana kuliko muziki ya aina hiyo yenye utasikia katika stesheni za redio.Katika utunzi wa nyimbo, Lecrae ana ujumbe mzuri kwako na mtu yeyote." Albamu hii,hivi sasa(Januari 2010),imekuwa katika chati ya BillBoard ya albamu za Kikristo kwa wiki 66.[13]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.