mwamba uliyeyushwa ulifukuzwa na volkano wakati wa mlipuko From Wikipedia, the free encyclopedia
Lava (kutoka jina la Kiingereza lenye asili ya Kilatini lava, wakati mwingine pia zaha[1]) ni mwamba ulio katika hali ya kiowevu kutokana na joto kali. Chini ya uso wa dunia mwamba joto wa kuyeyuka huitwa "magma" badala ya lava. Sawa na magma yenyewe lava inaweza kuwa nzito kama ujiuji au nyepesi kama majimaji.[2] .
Lava inatoka nje kwa kawaida wakati wa mlipuko wa volkeno. Inaweza kutoka pia katika ufa kwenye ganda la dunia.
Wakati wa kutoka hali yake ni kiowevu yenye halijoto kati ya 600°C hadi 1200°C. Ndani ya shimo la kasoko ya volkeno lava inaweza kukaa kama ziwa la kuchemka.
Ikitoka nje ya kasoko inaweza kuwa kama mto wa moto. Mwendo wake hutegemea na mnato wake yaani kama hali yake ni zaidi majimaji au ujiuji. Kadiri inavyoenea mbali na kasoko inapoa na kuwa mwamba.
Ikipoa inaganda na kuwa mwamba imara.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.