From Wikipedia, the free encyclopedia
Kuzi, dagaa, makame kuoza au mambanguma ni samaki za baharini na maji baridi za familia Atherinidae katika oda Atheriniformes. Wanatokea katika kanda za wastani mpaka tropiki.
Kuzi | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kuzi milia-mipana (Atherinomorus lacunosus) | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 13 na spishi 74, 9 katika Afrika:
| ||||||||||||
Kuzi ni wadogo, spishi kubwa kabisa, kuzi wa Kalifornia (Atherinopsis californiensis), anafikia urefu wa sm 44 lakini wengi zaidi ni chini ya sm 20 na kadhaa hazikuandikwa kwa zaidi ya sm 5. Kwa kawaida mwili umerefuka. Hulka bainifu zinajumuiya mapezimgongo mawili yaliyojitokeza sana, lile la kwanza likiwa limeundwa kwa miiba kinamo na lile la pili likiwa na mwiba mmoja unaofuatiwa na tindi laini. Pezimkungu pia lina mwiba mmoja unaofuatiwa na tindi laini. Mapeziubavu huwa juu na hakuna mrabafahamu. Kuna mlia mpana wa rangi ya fedha mbavuni. Magamba ni makubwa kiasi.
Hula planktoni-wanyama. Spishi kadhaa, k.m. kuzi milia-mipana (Atherinomorus lacunosus), huvuliwa kibiashara.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kuzi (samaki) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.