Kuchamsitu ni ndege wadogo wa familia Phylloscopidae. Wanafanana na shoro, kucha na kuchanyika, na zamani wote waliainishwa pamoja katika familia Sylviidae. Spishi za Phylloscopus zina rangi ya kahawia au kijani mgongoni na nyeupe au njano chini. Zile za Seicercus zina rangi kali zaidi, kijani mgongoni na njano chini; zina milia kichwani na mviringo wa jicho mweupe au njano. Ndege hawa wanatokea misitu ya Afrika, Asia na Ulaya. Spishi zinazozaa katika kanda za halijoto ya wastani huhamia kusi, zile za Ulaya huenda Afrika. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo la kikombe ndani ya uoto mzito, mara nyingi karibu na ardhi. Jike huyataga mayai 2-7.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Kuchamsitu |
Kuchamsitu koo-njano |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Nusufaila: |
Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
|
Ngeli: |
Aves (Ndege)
|
Oda: |
Passeriformes (Ndege kama shomoro)
|
Familia ya juu: |
Sylvioidea (Ndege kama kucha)
|
Familia: |
Phylloscopidae (Ndege walio na mnasaba na kuchamsitu) Alström, Ericson, Olsson & Sundberg, 2006 |
|
Ngazi za chini |
Jenasi 2; spishi 16 katika Afrika:
- Phylloscopus Boie, 1826
- P. bonelli (Vieillot, 1819)
- P. budongoensis (Seth-Smith, 1807)
- P. canariensis (Hartwig, 1866)
- P. collybita (Vieillot]], 1817)
- P. fuscatus (Blyth, 1842)
- P. herberti (Alexander, 1903)
- P. ibericus Ticehurst, 1937
- P. inornatus (Blyth, 1842)
- P. laetus (Sharpe, 1902)
- P. laurae (Boulton, 1931)
- P. orientalis (C.L. Brehm, 1855)
- P. proregulus (Pallas, 1811)
- P. ruficapilla (Sundevall, 1850)
- P. sibilatrix (Bechstein, 1793)
- P. trochilus (Linnaeus, 1758)
- P. umbrovirens (Rüppell, 1840)
- Seicercus Swainson, 1837
|
Funga
- Phylloscopus bonelli, Kuchamsitu wa Bonelli (Western Bonelli's Warbler)
- Phylloscopus budongoensis, Kuchamsitu wa Uganda (Uganda Woodland Warbler)
- Phylloscopus canariensis, Kuchamsitu wa Kanari (Canary Islands Chiffchaff)
- Phylloscopus collybita, Kuchamsitu Sauti-mbili (Common Chiffchaff)
- Phylloscopus fuscatus, Kuchamsitu Mgongo-kahawia (Dusky Warbler)
- Phylloscopus herberti, Kuchamsitu Utosi-mweusi (Black-capped Woodland Warbler)
- Phylloscopus ibericus, Kuchamsitu wa Hispania (Iberian Chiffchaff)
- Phylloscopus inornatus, Kuchamsitu Nyusi-njano (Yellow-browed Warbler)
- Phylloscopus laetus, Kuchamsitu Uso-mwekundu (Red-faced Woodland Warbler)
- Phylloscopus laurae, Kuchamsitu wa Laura (Laura's Woodland Warbler)
- Phylloscopus orientalis, Kuchamsitu Mashariki (Eastern Bonelli's Warbler)
- Phylloscopus proregulus, Kuchamsitu Kiuno-njano (Pallas's Leaf Warbler)
- Phylloscopus ruficapilla, Kuchamsitu Koo-njano (Yellow-throated Woodland Warbler)
- Phylloscopus sibilatrix, Kuchamsitu Mpigamluzi (Wood Warbler)
- Phylloscopus trochilus, Kuchamsitu wa Ulaya au Kapi (Willow Warbler)
- Phylloscopus umbrovirens, Kuchamsitu Kahawia (Brown Woodland Warbler)
Arctic warbler
Sulphur-bellied warbler
Radde's warbler
Pale-legged leaf-warbler
Greenish warbler
Whistler's warbler