Kiyiningayi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiyiningayi kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wayiningayi katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiyiningayi ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiyiningayi kiko katika kundi la Kimariki.