Kiyawarawarga
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiyawarawarga kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wayawarawarga katika majimbo ya Australia Kusini na Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiyawarawarga ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiyawarawarga kiko katika kundi la Kikarniki.