Kiyatay
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiyatay kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wayatay katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kiyatay, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiyatay kiko katika kundi la Kipama. Wengine hukiangalia kama lahaja ya Kigudang.