Kiyardliyawarra
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiyardliyawarra kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wayardliyawarra katika jimbo la Australia Kusini na New South Wales. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kiyardliyawarra, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiyardliyawarra kiko katika kundi la Kiyarli.