Kiyandjibara
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiyandjibara kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wayandjibara katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiyandjibara ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiyandjibara kiko katika kundi la Kimariki.