Kiyan-Nhangu
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiyan-Nhangu (au Kinhangu) ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wayan-Nhangu katika jimbo la Northern Territory. Mwaka wa 2005, kulikuwa na wasemaji wa Kiyan-Nhangu saba tu, na lugha imo hatarini mwa kutoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiyan-Nhangu kiko katika kundi la Kiyolngu.