Kiyalarnnga
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiyalarnnga kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wayalarnnga katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kiyalarnnga, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiyalarnnga kiko katika kundi la Kigalgadungiki.