Kiwurrugu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwurrugu kilikuwa lugha ya Kiyiwaidjan nchini Australia iliyozungumzwa na Wawurrugu katika jimbo la Northern Territory. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kiwurrugu, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwurrugu kiko katika kundi la Kiyiwaidjiki. Wengine hukiangalia kama lahaja ya Kiiwaidja.