Kiwotjobaluk
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwotjobaluk kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wawotjobaluk katika jimbo la Victoria. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiwotjobaluk ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwotjobaluk kiko katika kundi la Kimariki.