Kiwik-Iiyanh
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwik-Iiyanh ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wawik katika jimbo la Queensland. Mwaka wa 1981, idadi ya wasemaji wa Kiwik-Iiyanh ilihesabiwa kuwa watu 40 tu, yaani lugha imekaribia kutoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwik-Iiyanh kiko katika kundi la Kipama cha Kati.