Kiwemba-Wemba
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwemba-Wemba kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wawemba-Wemba katika jimbo la Victoria. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kiwemba-Wemba, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwemba-Wemba kiko katika kundi la Kulin.