Kiwathawurrung
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwathawurrung (au Kiwathaurong) kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wawathawurrung katika jimbo la Victoria. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiwathawurrung ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwathawurrung kiko katika kundi la Kikulin.