Kiwarungu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwarungu (au Kiwarrongo) kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wawarungu katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiwarungu ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwarungu kiko katika kundi la Kimariki.