Kiwarlmanpa
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwarlmanpa ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wawarlmanpa katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kiwarlmanpa 47 tu, na lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwarlmanpa kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.