Kiwardandi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwardandi kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wawardandi katika jimbo la Australia Magharibi. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiwardandi ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwardandi kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi. Wengine hukiangalia kuwa lahaja ya Kinoongar.