Kiwangkumara
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwangkumara ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wawangkumara katika jimbo la Queensland. Mwaka wa 2004, shirika la AUSTLANG lilitoa ripoti kudai kwamba idadi ya wasemaji wa Kiwangkumara ni watu 100, wote wazee, yaani lugha ya Kiwangkumara imekaribia kutoweka. Wengine husema kwamba ilitoweka tayari. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwangkumara kiko katika kundi la Kikarniki. Wengine hukiangalia kuwa lahaja ya Kingura.