Kiwambaya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwambaya ni lugha ya Kimirndi nchini Australia inayozungumzwa na Wawambaya katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kiwambaya 89. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwambaya kiko katika kundi la Kibarkly.