Kiwajuk
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwajuk kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wawajuk katika jimbo la Australia Magharibi. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiwajuk ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwajuk kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi. Wengine hukiangalia kuwa lahaja ya Kinoongar.