Kiwadikali
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwadikali kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wayarli katika jimbo la New South Wales. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kiwadikali, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwadikali kiko katika kundi la Kiyarli.