Kiumpila
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiumpila ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Waumpila katika jimbo la Queensland. Mwaka wa 2005, kulikuwa na wasemaji wa Kiumpila 12 tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiumpila kiko katika kundi la Kipaman.