Kiumbuygamu
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiumbuygamu kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Waumbuygamu katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kiumbuygamu, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiumbuygamu kiko katika kundi la Kipaman.