From Wikipedia, the free encyclopedia
Vitomo, vyelwende, vitatange, vitogoo au vitubaku ni samaki wa baharini wa jenasi Paracanthurus na Zebrasoma katika familia Acanthuridae wa oda Perciformes ambao wanafanana na kangaja lakini wana pezimgongo na pezimkundu makubwa kama tanga.
Kitomo | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kitomo kahawia (Zebrasoma scopas) | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Kama kangaja vitomo wana miiba kwa umbo la vijembe, mmoja kwa kila upande wa msingi wa mkia ("mikia ya miiba"), ambayo ni mikali na hatari sana. Kwa sababu hii, samaki hawa pia wana rangi kali za onyo. Pezimgongo na pezimkundu ni makubwa, katika jenasi Zebrasoma hasa, na yanafanana na tanga. Mdomo mdogo una safu moja ya meno yanayotumika kwa kujilisha na miani. Mdomo wa spishi za Zebrasoma unatokeza sana.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kitomo kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.