Kithayore
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kithayore ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wathayore katika jimbo la Queensland. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kithayore 29 tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kithayore kiko katika kundi la Kipaman.