Kitagalaka
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kitagalaka ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Watagalaka katika jimbo la Queensland. Mwaka wa 2005, kulikuwa na msemaji mmoja wa Kitagalaka tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kitagalaka kiko katika kundi la Kipaman.