From Wikipedia, the free encyclopedia
Kisiwa cha Krismasi ni eneo dogo la Australia katika Bahari Hindi takriban km 500 upande wa kusini wa Jakarta, mji mkuu wa Indonesia, na 2,400 kaskazini kwa Australia yenyewe.
Territory of Christmas Island Kisiwa cha Krismasi | |
Lugha rasmi | Kiingereza, Kichina, Kimalay |
Makao makuu | Flying Fish Cove |
Utawala | Eneo la ng'ambo la Australia |
Gavana | Michael Jeffery |
Pesa | Dollar ya Australia |
Wimbo wa taifa | Advance Australia Fair |
Kuna wakazi 1,600 wanokalia vijiji kaskazini mwa kisiwa. Theluthi mbili za eneo lake ni hifadhi ya taifa kwa sababu ya mazingira yake ya pekee pamoja na mimea na wanyama wake wasiopatikana mahali pengine duniani.
Jina lake liliteuliwa kwa sababu nahodha Mwingereza William Mynors, aliyekuwa kati ya watu wa kwanza kuona kisiwa hicho, alifika huko siku ya Krismasi mwaka 1643. Wakati ule kisiwa kilikuwa bila watu.
Katika karne zilizofuata kisiwa kilitembelewa mara chache kwa sababu mwambao wake ni vigumu kukaribiwa kwa jahazi kubwa. Lakini baada ya kugunduliwa fosfeti kisiwani migodi ikaanzishwa na wafanyakazi kuhamia kutoka Singapur, China na Malaysia. Hao walikuwa mababu wa wenyeji wa leo.
Mwaka 1958 kisiwa kikakabidhiwa kwa Australia.
Kisiwa cha Krismasi ni mahali pa pekee kwa sababu kinaonekana hakikufikiwa na watu hadi karne ya 16 na hakukaliwa nao hadi mwisho wa karne ya 19. Hivyo spishi nyingine zimehifadhiwa zilizoharibiwa penginepo.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.