Kiritarungo
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiritarungo (au Kiritharngu) ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Waritarungo katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kiritarungo 32 tu, na lugha imo hatarini mwa kutoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiritarungo kiko katika kundi la Kiyolngu.