Kipunthamara
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kipunthamara kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wapunthamara katika jimbo la Victoria. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kipunthamara ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kipunthamara kiko katika kundi la Kikarniki. Wengine hukiangalia kuwa lahaja ya lugha ya Kingura.