Kipitjantjatjara
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kipitjantjatjara ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wapitjantjatjara katika majimbo ya Northern Territory, Australia Kusini na Australia Magharibi. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kipitjantjatjara 2660. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kipitjantjatjara kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.