Kipinjarup
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kipinjarup kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wapinjarup katika jimbo la Australia Magharibi. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kipinjarup ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kipinjarup kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi. Wengine hukiangalia kuwa lahaja ya Kinoongar.