Kipallanganmiddang
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kipallanganmiddang (au Kibalangamida) kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wapallanganmiddang katika jimbo la Victoria. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kipallanganmiddang, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kipallanganmiddang kiko katika kundi la Gippsland.