Kinyiyaparli
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kinyiyaparli ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wanyiyaparli katika jimbo la Australia Magharibi. Mwaka wa 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kinyiyaparli watatu tu, na lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kinyiyaparli kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.