Kinuosu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kinuosu ni lugha ya Kisino-Tibeti nchini Uchina inayozungumzwa na Wayi. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kinuosu nchini Uchina imehesabiwa kuwa watu milioni mbili. Pia kuna wasemaji nchini Vietnam, Laos na Uthai. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kinuosu iko katika kundi la Kingwi.