Kinugunu (Australia)
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kinugunu kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wanugunu katika jimbo la Australia Kusini. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kinugunu imetoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kinugunu kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi. Isichanganywe na lugha ya Kinugunu cha Kamerun.